
kwa Wi-Fi
Zima nishati ya eneo la ufikiaji (kipanga njia pasi waya) na uiwashe tena. Wazingatie watumiaji wengine ambao wanaweza kuwa wanatumia mtandao.
Bofya Maelezo, na kisha uchapishe ripoti ya muunganisho wa mtandao.
Kulingana na matokeo ya uchunguzi, chukua hatua za usahihishaji kwa kutumia moja ya viungo vifuatavyo.

Kwa LAN ya Waya
Zima nishati ya kitovu na uiwashe tena. Wazingatie watumiaji wengine ambao wanaweza kuwa wanatumia mtandao. Kagua muunganisho tena baada ya karibu dakika moja baada ya kuzima na kuwasha kitovu upya.
Hakikisha kebo ya Ethaneti imeunganishwa vizuri. Ikiwa taa ya hali ya muunganisho imezimwa, kagua hali ya taa kwa kuunganisha kwa kituo kingine au kubadilisha kebo ya Ethaneti. Ikiwa tatizo halijatatuliwa, badilisha kitovu.